Jumatatu, 29 Julai 2013

NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE



5 
Fuatana nami sasa tuendelee na mfululizo wa somo hili. Biblia katika kitabu cha Mithali 14:1 inasema ‘Kila mwanamke aliye na hekima huijenga nyumba yake: Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’. Tafsiri ya neno nyumba ni familia, naam na familia inajumuisha baba, mama na watoto endapo mmejaliwa. Hata hivyo katika hali ya kawaida watoto watalelewa katika msingi mzuri endapo ndoa husika imetengamaa. Ifahamike kwamba hili andiko si la wanandoa peke yao, bali hata wanawake wasio wanandoa wenye familia kama wajane, walezi nk linawahusu. Kwa kuwa hapa tunazungumzia habari za wanandoa nitalifafanua zaidi kutoka kwenye kona hiyo. Pia neno nyumba limetumika ili kutupatia urahisi wa kuelewa namna nyumba za kawaida zinavyojengwa ili tueguze dhana hiyo kiroho pia. Kwa lugha rahisi ndoa yako ni nyumba, hivyo ubora, uzuri na mvuto wa ndoa yako unategemea namna unavyoijenga daima kwa hekima.
Ni vizuri ukafahamu kwamba suala la ujenzi/maboresho ya ndoa yako ni jukumu la kila siku ya kuishi kwa ndoa yenu mpaka kifo kiwatenganishe. Kila mmoja katika ndoa ni lazima ahakikishe anasimama kwenye nafasi yake na kufanya yale yampasayo ili kuifanya ndoa yake kuwa bora zaidi. Endapo hakutakuwa na jitihada za wanandoa katika kuimarisha ndoa yao, Shetani atatumia fursa hiyo kuivuruga ndoa husika. Kujenga kunakozungumziwa hapa ni kule kuhakikisha ndani ya ndoa kuna mahusiano na mawasiliano mazuri baina yenu ambayo yatafanikisha kutekelezwa kwa kusudi la Mungu.
Ukweli wa ajabu na wa pekee
Ni ajabu sana kuona kwamba jukumu la ujenzi wa ndoa/nyumba amepewa mwanamke. Hii haina maana mwanaume hahusiki, hapana, bali ki-nafasi jukumu la ujenzi wa nyumba/ndoa ni la kwako mama. Kumbuka nilikueleza kwamba nafasi hizi tano za Mwanamke katika ndoa zinafanya kazi kwa pamoja na kwa kutegemeana. Katika nafasi hii ya ujenzi unapaswa kuhakikisha unajenga ndoa yako ili kuzuia kila ufa/fursa ambayo Shetani anaweza kutumia kuvuruga ndoa yako. Kumbuka katika hali ya kawaida kujenga ni kuimarisha/kuweka mazingira bora juu ya kile unachokithamini ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea. Naam nafasi hii inalenga kukusaidia uwe makini sana na kila kinachoweza kubomoa ndoa yake.
7
Suala la ujenzi wa ndoa ni endelevu kwa sababu siku zote adui anatafuta kubomoa ndoa yako. Ni lazima uwe makini kujua wapi ni mahali palipobomoka ambapo Shetani anapatumia sasa kuharibu ndoa yako au anaweza kutumia baadaye kuharibu ndoa yako, naam ukishajua kwa kutumia hekima, jenga ukuta imara ambao adui hawezi penya. Kama ndoa yako ina nyufa basi ni rahisi adui kupita kwenye hizo nyufa. Kumbuka hata  kama umemaliza kujenga kila kitu kwenye nyumba yako, bado kuna matengenezo ya mara kwa mara yanahitajika ili kuifanya nyumba yako kudumu katika hadhi inayostahili. 
Maeneo ya msingi katika kujenga ndoa yako
  • Utiifu kwa mumeo
Maandiko yanasisitiza sana wanawake kuwatii waume zao (Waefeso 5:22-24,                1 Petro 3:1). Mitume walindika maandiko haya ili kuwaonya wanawake kutokana na mienendo yao mbele za waume zao kitabia na hasa katika suala zima la utiifu. Bahati mbaya baadhi ya akina mama sio watiifu kwa waume zao na tena wengine wana dharau kubwa sana. Naam fahamu kwamba Mke si Mke bila Mume, na Mume si Mume bila Mke. Hata siku moja ndoa yako haiwezi kujengwa kwa kiburi au dharau kwa mumeo bali utakuwa unaumba jambo baya sana ndani ya mume wako.
Najua unaweza ukasema tabia za mume wangu ndiyo zinazifanya kumdharau, kumsema vibaya nk. Suala sio tabia zake, bali ni wewe kutumia hekima katika kukabiliana na tabia zisifofaa za mumeo kwa kuwa kumdharau ni kuendelea kubomoa na si kujenga, naam  ni kuendelea kuleta tatizo na sio kutatua tatizo. Umeshawahi kuwaza juu ya jambo hili kwamba, Mke anaagizwa kumtii mume wake kama vile kumtii Bwana. Imeandikwa katika Waefeso 5:22 ‘Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu’. Je ni kweli ndivyo unavyomtii Mumeo? Naam haijalishi mume wako yukoje usionyeshe dharau, mtiii tu, ni mume wako.
Mtume Petro anawaonya wanawake akisema ‘kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno’ (1Petro 3:1). Sijui kama wewe Msomaji unaona uzito uliopo kwenye mistari hii. Kwa lugha nyepesi utiifu wa mke kwa Mume utawafanya wengine kumwamini Yesu mnayemtumaini. Naam na upande wa pili, kukosa utiifu kwa mumeo kutawazuia wengine kumwamini Yesu, je unajua gharama ya kuwazuia wengine kumjua Kristo kwa sababu ya kukosa utiifu kwa mumeo (asomaye na afahamu siri hizi).
Wanaume kadhaa walioko kwenye ndoa wamekuwa wakiniambia kwenye suala la tabia hawajaona tofauti kati ya wanawake wasiokoka na waliokoka. Na kikubwa wanachosema ni kudharauliwa na wake zao. Hata kama katika hali ya kawaida mumeo anafanya mambo yanayopelekea wengine kumdharau wewe usifanye hivyo yeye ni kichwa chako (Waefeso 5:23).
Fahamu kwamba daharau ni sumu mbaya kwenye ndoa yako yako mama, jizuie kabisa. Naam utiifu ni kila kitu kwa Mwanume, binafsi nimegundua wanachotafuta wanaume kwa wake zao bila kujali elimu zao, uchumi wao nk ni utiifu, naam kumdharau mumeo ni kubomoa nyumba yako ni kumruhusu Shetani kuharibu ndoa yako, ni kumuingiza mume wako fikra za wanawake wengine tofauti na wewe.
  • Kutunza siri za mume wako
Katika kuijenga nyumba yako ni lazima ujifunze kutunza, kuhifadhi na kuficha mapungufu ya mumeo kwa wengine. Naam hiyo ndiyo hekima. Baadhi ya akina mama   bila hata kujali wanaongea na nani, wamekuwa wakieleza mambo ya ndoa yao na siri za waume bila hata kujua athari yake. Naam kufanya hivyoni kubomoa na si kujenga. Unawajibika kmtii na kumtunzia mumeo siri zake licha ya mapungufu aliyo nayo na uzidi kumwomba Mungu kwamba aiponye ndoa yako.
2
Naam na hata kama ni muhimu uwaeleze kwa lengo la kujenga basi ni muhimu kuwe na mipaka ya nani unazungumza naye na nini unawaweleza maana si kila kitu wanapaswa kujua cha wewe na mumeo. Katika kulisistiza jambo hili Paulo anawagiza Tito akimweleza kwamba awatumie Wazee wa kike wenye mwenendo wa utakatifu ‘Ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao, na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe’ (Tito 2:3-4).
  •  Matumizi ya kinywa chako
Mara kadhaa nimewasikia wanawake walioolewa wakisema maneno yasiyofaa kwa waume zao. Najua wengine ni kutokana na hasira na wengine kutokana na mfululizo wa matukio yasiyofaa ya mumewe. Nimesikiia wanawake wakiwaaita waume zao wajinga, wapumbavu, na mengine ambayo nisinependa kuandika hapa. Ninachotaka ukijue ni hiki, imeandikwa Mtu atashiba kwa matunda ya kinywa chake.
Tambua kwamba mume wako naye ana nafasi zake kama mwanandoa kwako, na nafasi moja wapo ni kuwa kichwa cha mwanamke. Sasa kila baya unalotamka kwake maana yake unaliumba kwenye kichwa chako mwenyewe na hivyo tarajia mabaya na uharibifu kwenye ndoa yako. Najua utaniambia Patrick kuna mambo yanaudhi sana na hayavumiliki, na mimi nitakujibu ni kweli lakini namna ya kushughulika nayo ni wewe kutumia hekima kama mjenzi na kuiponya ndoa yako na si kumesema vibaya.
Fahamu pia kwamba katika ulimwengu wa roho kuna pepo ambao kazi yao ni kufuatilia maneno/mawazo mabaya ambayo mtu anayanena ili kuyaumba yatimie. Mfano ukiwa na wazo kwamba kwamba Mume wangu si mzuri uwe una uhakika kuna pepo watakuja juu yako na kuhakikisha siku zote wana kufanya umuone mume wako mbaya.
Je hujasoma Zaburi 36: 4 inasemaje ‘Huwaza maovu kitandani pake, hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii”. Naam tafsiri yake ni kwamba hali ya sasa ya mtu huyo ni matokeo ya mawazo yake, naam mwanandoa huyu amewaza na kunena mabaya juu ya mume wake, na kwa sababu hiyo ameiingiza ndoa yake kwenye mabaya. Naam ni lazima ujifunze kunena mananeo yenye kuijenga ndoa yako na si kubomoa, ndivyo na nafsi yako, fikra zako zitakapokiri hivyo, naam ndivyo na BWANA Mungu naye atahakikisha hayo yanakujia.
  •  Msamaha (kusameheana)
Ndoa nyingi leo zinashida kwa sababu ya wanandoa kushindwa kusameheana.  Ni kweli kwenye ndoa kuna mambo mengi ambayo katika hali ya kibinadamu yanaweza kukufanya ushindwe kusamehe, nami kama Mwalimu sina budi kukufundisha kile ambacho neno la Mungu limeelekeza. Kumbuka imeandikwa tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote… (Waebrania 12:14). Naam watu wote wa kwanza akiwa na mumeo, hatutegemei uwe na mahusainao mazuri na watu wa nje, wakati mume wako hutaki kumsamehe, utakuwa unajidanganya nafsi yako.
8
Hivyo bila kujali Mumeo amefanya kosa ganii hakuna namna ni lazima ujifunze kusamehe na kusahau. Hii ni kwa sababu kutokusamehe ni kumpa Ibilisi nafasi ya kuendelea kuwavuruga. Si hivyo bali usitegemee kwamba hata maombi yenu nyote wawili yatakuwa yanasikilizwa. Maana kwa kushindwa kwako kusamehe una haribu mahusiano na Mungu (Mathayo 6:14) na kwa mwanaume kwa kushindwa kwake kukaa kwa akili na wewe kama mke, maandiko yanasema maombi yake hayatasikilizwa. Je unategemea nini kitatokea kama hautakuwa tayari kumsamehe.
  •  Kujali mahitaji ya mwenzako (tendo la ndoa)
Paulo Mtume aliwaandikia hivi wanandoa wa Korinto ‘Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu’ (1Wakorinto 7:1-5).
Kimsingi andiko hili linalenga wanandoa wote wawili, bali kwa kuwa ujumbe huu ni maalum kwa wanawake nitaandika zaidi upande wa mwanamke. Biblia iko wazi kwamba kwa sababu ya zinaa (tendo la ndoa) kila mume awe na mke wake mwenyewe. Moja ya sababu muhimu za wewe kuolewa ni ili kumtosheleza mumeo kwa habari ya tendo la ndoa kama ilivyo na kwako pia.   
Kwa wanandoa wengi haja ya tendo la ndoa inatofautina, hata hivyo mara nyingi uhitaji wa tendo la ndoa kwa Mwanaume uko juu kuliko ilivyo kwa mwanamke. Hata hivyo kila mmoja ana – muhitaji mwenzake ili kutoshelezwa katika hitaji hili muhimu. Baadhi ya wanawake kwa kujua ukweli huu na tofauti hii ya uhitaji wa tendo la ndoa, kwa kutokufikiri athari zake kwa wenzi wao, kwao binafsi na ‘future’ yao huwanyima waume zao haki yao ya tendo la ndoa hasa pale wanapokuwa wametofautiana juu ya jambo fulani. Mbaya zaidi wapo akina mama ambao wakikasirika huwanyima waume zao haki hii ya msingi kwa muda mrefu kwa mfano mwezi mmoja, minne, hata zaidi ya mwaka na wanaishi nyumba moja na wengine wanalala kitanda kimoja.   
Mume wako akijua kwamba unatumia ugomvi/tofauti zenu au hata kwa makusudi kumnyima haki yake ya tendo la ndoa, na jambo hilo likawa endelevu uwe na uhakika taratibu unaanza kuharibu ndoa yako. Maana, Shetani ni mzuri sana wa kutumia nafasi ambazo wana wa Mungu wanampa. Ndani ya mume wako yataingia mawazo mabaya (Ezekieli 38:10) na kumweleza ‘je mbona kuna wanawake wengi, ni suala la kwenda kumaliza haja yako kwa mwanamke yoyote mwingine’. Wazo jingine pia litamwambia kwa nini huyu mwanamke akutese kiasi hiki, kwa nini usiwe na nyumba ndogo nk. Uwe na uhakika endapo mumeo ameokoka, hofu ya Mungu ndani yake ndiyo itakayomzuia kufanya mambo haya lakini ukimuuliza taratibu atakuambia mawazo haya hunijia mara kwa mara unaponinyima haki yangu ya tendo la ndoa.
6
Naam, hata kama hatafanya hayo, uwe na uhakika kwamba tayari kwenye ufahamu wake umeshapanda mbegu mbaya na itaendelea kukua endapo utaendelea na tabia yako ya kumnyima haki yake. Ndiyo, usishangae siku moja kukuta mumeo ametoka nje ya ndoa, usikimbilie kumlaumu Shetani, maana wewe ndiye ulifungua mlango na kumkaribisha. Nakumbuka mwanandoa mmoja (Mwanaume) alisema hizi ndoa za Kikristo zinatutesa sana wanaume, na zinawafanya hawa wanawake wajisahau sana, kwa kuwa wanajua Biblia imetuzia kuoa mke zaidi ya mmoja. Naam ilibidi nitumie muda mwingi kurejesha ufahamu wa huyu ndugu kwenye msingi wa ki-Mungu kwa kuwa nilijua tayari kuna wazo lilishaingia moyoni mwake na nilijua wapi linampeleka.
Nimeandika jambo hili kwa kirefu kwa sababu mara nyingi sehemu kubwa ya kesi za wanandoa inapofika kwenye suala la unyumba, wanawake ndio wanao – wanyima waume zao. Naam nakiri hata wanaume wapo lakini ni mara chache sio kama ilivyo kwa wanawake. Mwanamke sikia, kitendo cha Mungu kukupa huyo mume ni heshima ya pekee sana kwamba ni wa kwako pekee yako. Ukitaka kujua gharama yake waulize wanawake ambao wana ‘share’ mume namna inavyowagharimu kihisia, kifikra na kimaisha. Naam ni lazima ujifunze kujali na kutimiza mahitaji ya mwenzi wako vinginevyo unafungua mlango kwenye ufahamu wa mumeo na kumwambia angalia kule nje kuna wanawake wengine (Asomaye na afahamu).
Ukweli ni kwamba kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea wanawake kwenye ndoa kufanya hivyo, ila ushauri wangu ni kwamba, uamuzi wa namna hii (kumnyima tendo la ndoa mumeo) ni wa kuharibu na si kujenga. Hivyo haijalishi huyo baba kakukosea nini (labda ziwe issue za kiafya), suala la tendo la ndoa kwake ni muhimu sana na ni haki yake, kutokumpa haki yake ni kukaribisha Shetani kwenye ndoa yako. Naam ni vizuri mka-hakikisha kwamba tofauti zenu zote mna – zimaliza kabla hamjaingia kulala, itawasaidia sana.

Ushawishi katika kuomba msamaha!



KUKOSEA katika maisha ya binadamu ni kawaida. Ni sehemu ya maisha yake. Tena inaaminika kwamba, kukosea ni kujifunza, maana kosa utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika uhusiano na wapenzi wetu, mara kadha wa kadha tumejikwaa na kuwakosea.
Hakuna cha ajabu. Ni kawaida kabisa, lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna gani tunajifunza kupitia makosa. Ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti hizo. Maana unaweza kuwa hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe, lakini wimbo huo ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku.
Lakini pia, wapo ambao kwa bahati mbaya, bila matarajio yao wanajikuta wakiwa wamewaudhi wapenzi wao. Ni bahati mbaya na yawezekana kabisa wanaumia sana mioyoni mwao, lakini wakashindwa jinsi ya kumaliza ‘bifu’ hilo katika penzi lake.
Siku zote mkosewa hukosa raha, hupoteza hamu ya kukutana na mpenzi wake lakini kubwa zaidi, hujishusha/hukushusha thamani ya mapenzi yake kwako. Lakini mkosewa huyo huyo, akioneshwa kwamba makosa yaliyofanyika hayakuwa ya makusudi na kutumia njia bora za kufikisha hisia zako kwake, hujisikia amani na hali yake kurejea kawaida.
Hapa naita ni ushawishi wa kuomba msamaha. Huwezi kujua njia bora ya kuomba msamaha kama utakosa kitu kinachoitwa ushawishi. Rafiki zangu, yawezekana ukawa upo katika kipindi cha matatizo na mpenzi wako na hujui jinsi ya kuweka mambo sawa.
Wakati mwingine huna tatizo, lakini kwa sababu upo kwenye uhusiano basi si ajabu mambo kwenda mrama siku moja. Hapa chini, nimekuandalia mambo matano muhimu ya kuzingatia unapokuwa umekwenda kinyume kidogo kwa mpenzi wako.
Weka ubongo wako wazi, kuruhusu somo hili kichwani mwako, ambalo litakuwa hazina yako na mwongozo katika uhusiano wako. Kitu kikubwa ukumbuke, kukosea ni kawaida. Inatokea kila siku katika maisha yetu, hilo litoshe kukupa umuhimu wa kufuatilia kwa makini somo hili. Karibu darasani marafiki.
JAMBO LA KWANZA
Tafakari ukubwa wa kosa; Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwa ababu hujamwambia chochote, naye hana raha na wewe. Hana amani ya moyo.
Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo. Kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani?
Mathalani unaweza kuwa ulimuudhi kwa ababu alikupigia simu zaidi ya mara kumi bila kupokea, akakasirika. Hili ni kosa dogo. Lakini yawezekana alikuta meseji ya mapenzi kwenye simu yako au alikufumania; Haya ni makosa makubwa. Tafakari na ujue ukubwa wa kosa lako.
JAMBO LA PILI
Jutia kwa moyo; Hii ni kwa ajili yako wewe mwenyewe. Rafiki zangu, kutakuwa hakuna maana yoyote kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo, kama msamaha wako haujatoka moyoni.
Ukiwa peke yako, jiaminishe kwamba umekosea na kwa hakika unahitaji kusamehewa.
Jutia ndani ya moyo wako, kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi kwamba hutarudia tena. Hili ni zoezi la Kisaikolojia, ambalo litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi wako kwa ajili ya kuomba msamaha.
JAMBO LA TATU
Mpe ukweli; Omba kukutana naye. Yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini hapa jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wa karibu sana na yeye. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.
Mweleze ukweli wa kosa lako, onesha jinsi linavyokutesa na kukusumbua. Usijaribu kuongea uongo wowote katika suala hili. Kuwa mkweli. Jutia kwa moyo, aone majuto yako usoni mwako.
Mwambie jinsi unavyoteseka na jinsi msivyo katika maelewano mazuri. Kauli yako ya ukweli, hisia zako wakati wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka katika mazingira mazuri ya kuweka mambo sawa.
JAMBO LA NNE
Ahidi kutorudia makosa; Bila shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini, uwezekano wa kusamehewa ni mkubwa sana. Hili ndiyo matarajio yangu, naamini hata wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie mpenzi wako kuwa hutaruidia tena.
Mwambie kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya tena asiwe na furaha. Hakuna uchawi ni maneno tu!
JAMBO LA MWISHO
Mfanyie kitu maalum; Hapa unatakiwa kufanya kitu maalumu kwa ajili ya mpenzi wako, ukionesha kwamba umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu utakachokifanya hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema awali.
Mathalani unaweza kutoka naye na kwenda kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa mahaba mazito kama shukrani kwake. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kulingana na uwezo wako kifedha. Fanya vyovyote ili kosa lile lisahaulike moja kwa moja!
Yes! Kila kitu kipo mikononi mwako? Bado hujasamehewa tu? Labda awe tayari ana maamuzi mengine, vinginevyo hapo hapindui!

SALAMU ZA IDD EL FITRI KUPITIA BLOG HII


Mpendwa Msomaji, Ikiwa utapenda kutuma salamu za Idd el Fitri kwa ndugu na marafiki, basi harakisha kutuma salamu zako kupitia blog hii
Msikiti uliopo Madina,Saudi Arabia Msikiti uliopo Madina,Saudi Arabia

Maandamano ya kuipinga serikali ya kiislamu nchini Tunisia yazidi kushika kasi


Mazishi ya kiongozi wa upinzani aliyeuawa nchini Tunisia, Mohammed Brahmi

Polisi nchini Tunisia wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya waandamnaji katika barabara za mji wa Sidi Bouzid wanaondamana kutaka serikali ya Kislamu kuondoka madarakani. Waandamanaji hao wameendelea kupaza sauti zao kwa zaidi ya juma moja sasa baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Mohammed Brahmi.

Wafanyakazi waliokuwa wanakwenda kazini siku ya jumatatu walizuiliwa kuingia sehemu zao za kazi na waandamanaji hao waliowataka kujiunga nao ili kuendelea kushinikiza chama cha Ennahda kuondoka madarakani.
Wakati makabiliano hayo yakiendelea, viongozi wa serikali wamekuwa wakikutana kwa dharura kujadili mustakabali wa maandamano hayo ambayo yanayofiwa huenda yakawa makubwa kama yale yaliyoingusha serikali ya Rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali.
Mohammed Brahmi anakuwa kiongozi wa pili wa upinzani nchini humo kuuawa baada ya kiongozi mwingine Chokri Belaid kupigwa risaisi na kuuawa nyumbani kwake mapema mwaka huu.
Upinzani nchini Tunisia umeendelea kuitumu serikali kwa kuwauawa viongozi wao tuhma ambazo serikali imeendelea kukanusha.

Zoezi la kuhesabu kura za urais wa Mali laendelea kwa amani

Wapiga kura waliojitokeza kumchagua Rais mpya wa Mali

Zoezi la kuhesabu Kura nchini Mali limeendelea baada ya kutamatika kwa upigaji kura za Uraisi. Mamilioni ya wananchi walijitokeza kushiriki zoezi hilo siku ya jumapili na kutupilia mbali vitisho vya uvunjifu wa amani vilivyotolewa na kundi la wapiganaji wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo MUJAO.

Waangalizi wa kimataifa wamesifu idadi kubwa ya wapiga kura waliojitokeza huku kukiwa na ulinzi mkali katika vituo mbali mbali nchini humo, kuanzia katika mji mkuu Bamako.
Mpaka asubuhi ya jumatatu hakukuwa na uvunjifu wa amani ulioripotiwa kujitokeza dhidi ya wapiga kura wala wasimamizi wa zoezi hilo.
Raia wa Mali walitakiwa kumchagua raisi wao miongoni mwa wagombea 27 walioidhinishwa na tume ya uchaguzi na mshindi wa kinyang'anyiro hicho ndiye atakayefanikisha uundwaji wa serikali ya muungano wa kitaifa.
Taarifa toka nchini humo zinadokeza kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa hilo Ibrahim Boubacar Keita anaongoza katika matokeo ya awali yaliyokwishahesabiwa katika baadhi ya vituo.
Aidha Waziri Modibe Sidibe ambaye naye ni Waziri Mkuu wa zamani na Soumaila Cisse ambaye ni Waziri wa zamani wa fedha wanaonyesha dalili za kupata uungwaji mkono katika kura hizo.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutolewa na wizara ya mambo ya ndani siku ya jumanne.
Endapo hakutakuwa na mgombea aliyeibuka na kura nyingi zaidi basi duru la pili la uchaguzi huo litafanyika tarehe 11 ya mwezi Agosti na kuwashirisha wagombea waliopata zaidi ya asilimia 50.

Bunge la Kiarabu lalaani mauaji ya Tunisia na Libya


Bunge la nchi za Kiarabu limelaani mauaji ya kisiasa yaliyotokea huko Tunisia na Libya na kueleza kuwa, utatuzi wa kisiasa ndio njia bora zaidi ya kuhitimisha mgogoro ulioikumba Misri.
Spika wa Bunge la nchi za Kiarabu Ahmad bin al Jarwan ametoa taarifa akilaani vikali kuuawa viongozi wa upinzani huko Tunisia na Libya. Al Jarwan ameongeza kuwa, kuuawa shakhsia wa kisiasa kunapasa kukomeshwa kwa sababu kitendo cha kuuwa mtu ni jinai dhidi ya ubinadamu. Ahmad bin Muhammad al Jarwan ameyataka makundi na vyama vyote vya kisiasa huko Misri kuacha kuchochea machafuko na badala yake kufanya mazungumzo na kutafuta njia ya kisiasa ili kurejesha utulivu na umoja nchini humo.
Vilevile amewaomba viongozi wa serikali ya mpito ya Misri kuunga mkono maandamano ya amani ya wananchi na kulinda haki yao ya uhuru wa kujieleza.

Maandamano yachacha Misri

 
Waandamanaji wamekita kambi kutaka Morsi aachiliwe
Maelfu ya wafuasi wa kiongozi aliyeondolewa madarakani nchini Misri, Mohammed Morsi wameandamana usiku kucha hadi karibu na kambi moja ya kijeshi mjini Cairo kabla ya kurudi na kukita kambi kando ya msikiti mmoja.
Hata hivyo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na jeshi licha ya onyo kutoka kwa waziri wa maswala ya ndani nchini humo Mohammed Ibrahim, kwamba mamlaka itajibu vitisho vyovyote dhidi ya usalama kutoka kwa waandamanaji hao.
Zaidi ya wafuasi 70 wanaotaka Morsi kurejeshwa madarakani waliuawa baada ya ghasia kuzuka kati ya waandamanaji na vikosi vya jeshi hapo Jumamosi.
Waziri wa mambo ya nje nchini humo amezitaka pande zote kwenye mgogoro huu kujizuia na kusababisha ghasia, siku moja baada ya ghasia nchini humo kusababisha vifo vya watu 70.
Kwenye mahojiano na BBC,Nabil Fahmy alisema kuwa pande zote zinapaswa kujizuia na kuchochea ghasia kwa kutumia vurugu.
Mnamo siku ya Jumamosi, wafusai wa aliyekuwa rais Morsi, walikabiliana na polisi pamoja na maafisa wengine wa usalama huku maelfu ya waandamanaji hao wakiendelea kupiga kambi.
Wakati huohuo, rais wa muda Adly Mansour amemuamuru waziri wake mkuu kulikabidhi jeshi mamlaka kuwakamata raia.
Mwandishi wa BBC Jim Muir ambaye yuko mjini Cairo anasema kuwa baadhi ya watu wanaiona hii kama dalili ya wasiwasi na mwanzo wa serikali kuanza kupambana na waandamanaji waliokita kambi katika msikiti wa Rabaa al-Adawiya .
Waziri wa mambo ya ndani, Mohamed Ibrahim amekuwa akionya mara kwa mara kuwa waandamanaji hao watatawanyishwa karibuni , ingawa waandamanaji wenyewe wanasema hawatabanduka.
Kulikuwa na ghasia siku ya Jumapili, huku watu wawili wakiuawa mjini Cairo.
Mwishoni mwa wiki wapiganaji kumi wa kiisilamu waliuawa na jeshi katika Rasi ya Sinai ambako wamezidisha mapigano kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Mena.

Keita aongoza matokeo ya awali nchini Mali


Duru za habari zinaripoti kuwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita anaongoza kwenye matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili ya jana.
Habari zaidi zinasema huenda Keita akashinda uchaguzi huo katika duru ya kwanza. Maelfu ya wafuasi wake wameanza kukusanyika kwenye makao makuu ya chama cha Rally for Mali kinachoongozwa na mwanasiasa huyo. Maelfu ya wafuasi wengine pia wamekusanyika nyumbani kwa Keita mjini Bamako.
Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani mkali unaonekana ni kati ya Ibrahim Keita mwenye umri wa miaka 69 na waziri wa zamani wa fedha, Soumaila Cisse mwenye umri wa miaka 63. Uchaguzi huo wa Mali ni wa kwanza wa kidemokrasia tangu kutokee mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Amadou Toumane Toure mwanzoni mwa mwaka uliopita.

Siwezi kuwahukumu mashoga,asema Papa Francis

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amesema hawezi kuwahukumu mashoga, lakini akalaani kampeni ya kuhalalisha ushoga akiiita tatizo kubwa. Vile vile Papa Francis amesema kanisa halina budi kuwapa wanawake majukumu makubwa, ingawa amesema kuwa milango ya wao kuwa mapadre imefungwa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege yake akitokea Brazil kurudi Roma, Papa Francis alisema kuwa shoga sio tatizo, tatizo kampeni ya kuuhalilisha. Alisema kama mtu ni shoga na anamtafuta mungu kwa nia ya dhati, basi yeye hawezi kumhuku.
Kiongozi huyo wa wakatoliki ulimwenguni alijibu maswali kuhusu mtu aliyemteuwa kuongoza banki ya Vatican yenye matatizo, Battista Ricca, ambaye licha ya uteuzi huo anasakamwa na shutuma ya kuwa na uhusiano wa kingono na shoga. Papa amesema aliagiza uchunguzi mfupi juu ya madai hayo, lakini hakukua na ushahidi wowote dhidi ya mtu huyo

Jumapili, 28 Julai 2013

Wafuasi wa Morsi waendelea kupiga kambi.

i

Wafuasi wa rais Morsi

Wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohammed Morsi wameendelea kupiga kambi katika msikiti wa Rabaa al-Adawiya mashariki mwa mji mkuu wa Cairo,

Ikiwa ni siku moja tu baada ya ghasia kali kuzuka.
Waandamanaji hao wameweka vizuizi katika kambi yao na kuapa kutoondoka licha ya mapambano kati yao na vikosi vya ulinzi na usalama.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesitikitishwa na ghasia zinazoendelea nchini Misri.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,bwana Kerry amesema kuwa wakati huu ni muhimu sana kwa taifa hilo na akatoa wito kwa serikali hiyo kuheshimu haki ya raia kuandamana kwa amani na uhuru wa kujieleza.
Mwandishi wa BBC anasema hali sasa imetulia kiasi licha ya vurugu kutokea katika viunga vingine vya mji wa Cairo.

Wafungwa 1200 watoroka kutoka gereza la Benghazi nchini Libya


Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Libya Ali Zaidan amesema wafungwa 1200 wametoroka kutoka gereza la Benghazi nchini Libya.
Bw. Zeidan amesema gereza hilo lilishambuliwa na wakazi wa huko ambao hawapendi kuishi karibu na gereza. Kikosi maalum ambacho kina uwezo wa kudhibiti hali ya huko, kilishindwa kuwazuia wakazi walipokuwa wakifungua mlango wa gereza hilo baada ya kupewa amri ya kutowafyatulia risasi wakazi hao. Bw. Zeidan amesema wafungwa waliotoroka watasakwa kote nchini humo, na vituo vya ukaguzi mpakani vitatumiwa orodha ya majina ya wafungwa hao.

Uchaguzi wa urais nchini Mali


Duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Mali imefanyika leo tarehe 28 Julai nchini humo. Viongozi wa nchi hiyo wametabiri kuwa, karibu watu milioni saba wameshiriki kwenye uchaguzi wa leo. Katika duru hiyo, wagombea 27 wamechuana vikali kuwania nafasi hiyo. Hii ni katika hali ambayo Ibrahim Boubacar Keita, waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo na Soumaila Cisse waziri wa zamani wa fedha, wanatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuweza kushinda katika uchaguzi huo. Karibu askari 6300 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamechukua jukumu la kulinda usalama katika uchaguzi huo. Zaidi ya hayo, askari 3200 wa Ufaransa pia bado wako nchini humo, kwa kile kinachodaiwa ni kuvisaidia vikosi vya Umoja wa Mataifa katika kazi zao za kulinda amani. Aidha chanzo kimoja cha usalama nchini Mali kimetangaza habari ya kuweko askari wa kujitolea wapatao 4500, ambao wameandaliwa na serikali ya Bamako kwa minajili ya kudhaminia usalama katika zoezi zima la uchaguzi huo. Habari kutoka Mali zimearifu kwamba, viongozi wengi wa nchi hiyo, wamepiga kura zao mjini Bamako huku wengine wakipiga kura katika vituo rasmi vilivyosimamiwa na polisi ya nchi hiyo. Hata hivyo pamoja na kuwepo askari wote hao, bado kuna wasi wasi wa kutokea machafuko ya baada ya uchaguzi nchini humo. Jana Harakati ya Umoja na Jihadi Magharibi mwa Afrika 'MUJAO', ilitoa vitisho dhidi ya serikali ya Bamako na kuwataka wananchi kutokwenda kupata kura. Aidha harakati hiyo, ilitishia kuwa, wapiganaji wake watafanya mashambulizi dhidi ya vituo vya kupigia kura, hususan katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Tangu wiki iliyopita, mji wa Kidal wa kaskazini mwa Mali, umekuwa ukishuhudia machafuko yanayofanywa na wapinzani ili kuvuruga hali ya usalama nchini humo. Kufichuliwa bomu la kutengenezwa kienyeji karibu na soko la mji wa Kidal, kumezitia khofu nyoyo za raia wa kawaiada kuhusiana na usalama wa eneo hilo. Aidha utekaji nyara wa watu ni suala lingine lililozua khofu kubwa katika uchaguzi wa leo. Wiki iliyopita, meya wa mji wa Kidal na mmoja wa wafanyakazi wake, walitekwa nyara. Wapiganaji wa Harakati ya Kitaifa ya Azawad waliisimamisha gari ya meya huyo, katika lango la kuingilia mji huo na kuwateka nyara watu wawili kati ya wanne waliokuwamo ndani ya gari hilo akiwemo meya huyo. Pamoja na hayo yote lakini weledi wa mambo wanaamini kwamba, kufanyika uchaguzi wa leo, ni hatua moja mbele kuelekea kwenye utawala mpya kikatiba nchini humo. Si vibaya kukumbusha hapa kwamba, uchaguzi wa leo umefanyika ikiwa ni baada ya kupita miezi sita, tangu Ufaransa ilipoingilia kijeshi mgogoro wa Mali. Aidha uchaguzi wa leo umefanyika katika hali ambayo, zaidi ya watu 500,000 wanaishi kwenye kambi za wakimbizi wa ndani na inaaminika hawakupata fursa ya kujiandikisha kama wapiga kura. Wakosoaji wanasema kuwa, jamii ya kimataifa imeishinikiza Mali kufanya uchaguzi katika hali ambayo nchi hiyo ilikuwa haijajiandaa kikamilifu kwa ajili ya zoezi hilo. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon amesema uchaguzi ndiyo njia pekee ya kurudisha demokrasia katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, rais ajaye nchini Mali atakuwa na majukumu makubwa na hatari, hasa kwa kuzingatia mgogoro na vitisho vya wapinzani wa kaskazini mwa nchi hiyo, umasikini mkubwa na kuzorota hali ya uchumi. Wakati huo huo, wachambuzi wengine wa mambo wanaamini kuwa, uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kwa serikali ya Bamako na ahadi kemkem za kuipatia nchi hiyo msaada wa Euro bilioni tatu, ni katika mambo yanayotia matumaini ya kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo.

Matukio ya Misri yanaonesha kina cha mwamko wa Kiislamu'


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, matukio ya nchini Misri yanaonesha kina cha mwamko wa Kiislamu katika nchi hiyo.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo jioni wakati alipoonana na wanachuo na wawakilishi wa asasi za kielimu, kiutamaduni, kisiasa n.k, za Vyuo Vikuu vyote vya Iran na kusisitiza kuwa, matukio yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa Misri yanaonesha kina na kilindi kirefu cha mwamko wa Kiislamu nchini humo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, mwamko wa Kiislamu haukuongozwa vizuri nchini Misri na kusisitiza kuwa, yanayotokea nchini Misri hivi sasa yanahuzunisha na kuumiza sana na hayo yote ni kutokana na kufanyika makosa katika kuongoza mwamko huo wa Kiislamu.
Pia amesema kutekeleza wajibu hakukinzani hata kidogo na wajibu wa kuangalia matokeo ya baadaye na inabidi kufuata njia sahihi kwa ajili ya kufikia kwenye matunda mazuri.
Habari zaidi kuhusu mkutano huo tutakuleteeni katika matangazo yetu yajayo, Inshaallah...

Ripoti: Ubaguzi wa rangi Ulaya bado ni tatizo sugu


Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Italia limesema kwenye ripoti yake kwamba, ubaguzi wa rangi barani Ulaya bado ni tatizo sugu. Shirika hilo linalojiita I CARE limesema tukio la hivi karibuni la kutupiwa ndizi waziri wa kwanza mweusi nchini humo limedhihirisha kuwa, ubaguzi wa rangi Italia na barani Ulaya kwa ujumla bado ni tatizo kubwa na lilanopaswa kukabiliwa vikali. Bi. Cecile Kyenge alitupiwa ndizi wakati akihutubia siku ya Ijumaa katika mji wa Cervia mkoani Ravenna, tukio linalonasibishwa na nyani au sokwe-mtu. Hii si mara ya kwanza kwa waziri huyo kukumbana na hujuma hiyo ya ubaguzi wa rangi. Miezi kadhaa iliyopita, Waziri Kyenge alizomewa na kundi la vijana mashariki mwa nchi hiyo na baadhi yao pia kumtupia ndizi

Syria yaitaka UN kuwachukulia hatua magaidi


Syria imeutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya jinai zilizofanywa na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za kigeni nchini humo, kufuatia kuuliwa kwa umati na magaidi hao, watu wasiopungua 123 huko katika mji wa Halab wa kaskazini mwa Syria. Shirika la habari la Syria (SANA) limeripoti kuwa, magaidi wenye silaha walioko nchini humo wameuwa watu wasiopungua 123 wengi wao wakiwa ni raia katika shambulizi walilolifanya huko Khan Assal, magharibi mwa mji wa Halab.  Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imemuandikia barua tofauti Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuutaka umoja huo uzizuie nchi zinazowaunga mkono magaidi hao baadhi yake zikiwa zinapakana na Syria, ili magaidi hao wasiendelee kufanya mauaji ya umati dhidi ya raia nchini humo. Barua hizo kwa Ban Ki Moon zimeeleza kuwa kundi hilo la magaidi la huko Syria linalojiita kwa jina la Brigedi ya Ansar al Khalifa, limekiri kuhusika na mauaji hayo ya Khan al Assal. Habari zinasema kuwa baada ya kuwauwa raia hao wa Syria, magaidi hao walikata miili ya wahanga na kuitupa katika shimo kubwa nje ya mji huo na pia kuichoma moto baadhi ya miili ya watu waliowauwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria pia imezikosoa vikali baadhi ya nchi kwa misimamo yao ya undumakuwili kuhusiana na mapambano dhidi ya ugaidi.  Barua hizo tafauti za Syria kwa Umoja wa Mataifa pia zimeitaka taasisi hiyo kubwa ya kimataifa kuchukua hatua za kweli za kupambana na ugaidi huko Syria.

Wanajeshi wa Syria wateka ngome za waasi


Televisheni ya al Alam imeripoti kuwa, wanajeshi wa Syria wamefanikiwa kuteka ngome za mwisho za makundi ya waasi katika eneo la al Khalidiyyah mjini Homs na kusema kuwa mapigano yanaendelea katika viunga vya mji huo kati ya wanajeshi na waasi.
Televisheni hiyo imeongeza kuwa, jeshi la Syria limefanikiwa kuukomboa msikiti wa Khalid bin Walid katika eneo la al Khalidiyyah huko Homs na kunukuu habari zisizothibitishwa kuwa sehemu hiyo ilikuwa ndiyo ngome ya mwisho ya waasi katika eneo hilo.
Mwandishi wa al Alam aidha amesema kuwa, mapigano makali yameendelea kwa wiki kadhaa katika eneo hilo na kuongeza kuwa, kufanikiwa jeshi la Syria kudhibiti eneo hilo ni sawa na kuwasafisha waasi katika mji wa Homs hasa Homs ya Kale.
Vile vile mwandishi wa al Alam amesema kuwa kundi moja la magaidi lilijaribu kuingia kwenye kituo cha umeme kwenye eneo la al Abasiyyin katika viunga vya Damascus lakini jeshi limelidhibiti kundi hilo kama ambavyo mapigano makali yanaendelea katika maeneo ya Qabun, Juwabir na Barzi.

Wanajeshi wa Misri wauwa wanamgambo kumi Sinai


Vikosi vya usalama vya Misri vimewauwa kwa risasi wanamgambo kumi waliokuwa na silaha na kufanikiwa kuwatia nguvuni wanamgambo wengine 20 katika oparesheni yao ya masaa 48 huko katika jangwa la Sinai. Afisa mmoja wa jeshi la Misri ameeleza kuwa, operesheni zilizofanywa na vikosi vya nchi hiyo huko kaskazini mwa Sinai kwa ajili ya kuwasaka wanamgambo imepelekea kuuawa wanamgambo kumi waliokuwa na silaha. Jangwa la Sinai ambalo liko kwenye mpaka wa Misri na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, limekuwa na likishuhudia mapigano kati ya watu wenye silaha wasiojulikana na vikosi vya Misri tangu apinduliwe Rais Muhammad Morsi wa nchi hiyo mwezi Julai mwaka huu.
Wanajeshi wawili wa Misri waliuawa Alhamisi iliyopita katika shambulio la lililofanywa na watu wenye silaha kwenye kituo cha upekuzi cha kijeshi karibu na mji wa Sheikh Zuweid huko katika jangwa la Sinai.
Wakati huo huo watu wawili wameuawa leo katika matukio mawili tofauti nchini Misri wakati wafuasi wa Muhammad Morsi rais wa nchi hiyo aliyeng'olewa madarakani na jeshi walipopambana na wapinzani wa rais huyo wa zamani wa Misri. Watu hao wawili wameuawa leo katika mji wa bandari wa Suez na katika mji wa Kafr el Zayat, kaskazini mwa nchi hiyo.

JACK WOLPER: NISIPOANGALIA, PRESHA ITANIUA

Na Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza kuwa, tatizo alilonalo la presha ya kushuka huenda siku moja likawa chanzo cha kifo chake kwani linapomjia, huwa katika hali mbaya sana.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Wolper alisema, tatizo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini likapungua lakini sasa limerejea na linamkosesha amani.
“Kwa kweli hili tatizo la presha ya kushuka nililonalo ipo siku litaniondoa duniani, unajua wakati  mwingine hali hiyo ikinijia natokwa na damu nyingi puani, huoni ni tatizo kubwa hili!” alisema Wolper

source global publishers

MSICHANA ANYONGWA NA MPENZI WAKE

 Bagamoyo Pwani
MSICHANA Rehema Athumani Mpendae, ameuawa kikatili kwa kunyongwa na mtu anayedhaniwa kuwa ni mpenzi wake huku chanzo cha kufanyiwa unyama huo kikiwa hakijulikani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu waliopanga katika nyumba moja na marehemu, wamekadiria kuwa Rehema alinyongwa saa 12 jioni kwenye nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Majani Mapana wilayani hapo.
Alisema baada ya polisi kupata taarifa walifika katika eneo la tukio na kukuta msichana huyo akiwa amedhalilishwa na kuuawa kinyama kisha wakamuita.
 “Baada ya kufika kwenye nyumba hiyo nikatakiwa na polisi kuingia ndani ili kujua kama kuna mtu katika chumba cha marehemu,” alisema Matata.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuingia ndani aliukuta mwili wa binti huyo ukiwa umelazwa kitandani bila ya nguo huku ukiwa umefunikwa, mdomoni akiwa amezibwa kwa kanga.
Mmoja wa wapangaji wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Fauzia Abdallah (20), alisema kuwa mara ya mwisho kumuona Rehema ilikuwa ni Ijumaa jioni ya Julai 19, mwaka huu.
“Siku hiyo ilipofika  jioni nilimsikia akizungumza kwa simu huku akimtaka mtu ambaye inaonekana alikuwa mpenzi wake na hakuwa mbali na hapa akimwambia amsubiri ili waonane.
“Alitoka ndani na baada ya muda nilimsikia akiingia na mtu ambaye alikuwa na sauti ya kiume lakini kwa sababu nilikuwa ndani kwangu nikiangalia TV, sikuweza kumuona au kumfahamu,” alisema Fauzia.
Alifafanua kuwa kama saa 12 hivi jioni alisikia wakiwa wanabishana lakini hakuweza kujua walibishania kitu gani na baadaye kukawa kimya na hawakuonana tena hadi aliposikia kesho yake kuwa ameuawa kikatili.

AMANDA, BWANA MISOSI WAMWAGANA

Na Gladness Mallya
HATIMAYE wale wapenzi waliong’aa hivi karibuni, mwigizaji Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ wanadaiwa kumwagana rasmi, Ijumaa limetonywa.
Tamrina Poshi ‘Amanda’ akiwa na mpenzi wake wanayedaiwa kumwagana naye, Emmannuel Rushau ‘Bwana Misosi’.
Habari kutoka chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wapenzi hao, zilieleza kuwa Amanda na Bwana Misosi walishamwagana kimyakimya ikiwa ni baada ya kushindwa kuelewana kitabia.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Amanda ili aelezee ukweli kuhusu habari hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli wameshaachana na hii ni baada ya kushindwana kitabia.
Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda.
“Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili  baada ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza kujuta,” alisema Amanda.
Kwa upande wake Bwana Misosi hakuweza kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa bali alianza kwa kujikanyagakanyaga
“Kwanza niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo,” alisema Misosi.

HII NI KALI YA MWAKA,,,joks sõidab ''autoga'' - Video Dailymotion

joks sõidab ''autoga'' - Video Dailymotion

LULU AZUA HEKAHEKA

Stori:Denis Mtima
MWIGIZAJI mahiri Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Jumatano iliyopita alizua hekaheka mtaani baada ya kutinga kwenye duka moja na watu kumtumbulia macho kwa kumshangaa.
Tukio hilo lilitokea kwenye duka hilo lililopo Sinza Afrika Sana ambapo staa huyo mwenye kesi ya madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa staa wa filamu za Bongo, marehemu Steven Kanumba, alitinga dukani hapo akihitaji huduma ya fedha kwa njia ya mtandao wa simu.
Baadhi ya watu waliokuwa wanapita jirani, walimkodolea macho Lulu huku kila mtu akisema lake. Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina, alisikika akisema:
“Ametulia siku hizi, tangu ametoka Segerea amekuwa mtulivu sana.”
Baada ya kuhudumiwa, Lulu alitoka lakini baadaye akagundua kuwa amesahau funguo ya gari, hali iliyomlazimu kurudi dukani.
Aliporudi dukani, aliiona funguo hiyo, akatoka na kwenda kwenye gari alilokuja nalo. Ndani ya gari hilo aina ya Toyota Mark II, alikuwa na mdogo wake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

sOURCE GLOBAL PUBLISHERS

WACHAZAJI WA MAN CITY WAKIFANYA MAZOEZI KWENYE WAKATI WA MVUACity in Hong Kong: TRAINING IN THE RAIN - Day 16,,,

TAZAMA MN UNITED WANAVYOJIVUNZA JINSI YA KUSLID UWANJANI

HIVI NDIVYO TAIFA STARS ILIVYONYOLEWA NA UGANDA THE CRANES NA KUSHINDA KWENDA CHAN

Wachezaji wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na Uganda Cranes wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mechi yao ya kufuzu kucheza Chan iliyofanyika kwenye uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala.


Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes'


Mchezaji wa Taifa Stars Aggrey Morris (katikati) akiwania mpira huku akizongwa na mabeki wa Uganda Cranes.Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Amri Kiemba akipongezwa na Mrisho Ngasa/ Aboubakar Salum 'Sure Boy' baada ya kushinda bao la kusawazisha dhidi ya Uganda Cranes



Washabiki wa Taifa Stars wakishangilia goli la kusawazisha..

Kiemba






MALOVEE YAMNG’ARISHA DAVINA

Halima Yahaya ‘Davina’.
Na Imelda Mtema
MWIGIZAJI Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amesema licha ya kuwa amejifungua hivi karibuni mtoto wa tatu lakini mahabati anayopata kwa mumewe, yanamfanya aonekane kama kigori.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni jijini Dar, Davina alisema amekuwa akiulizwa na watu wengi siri ya mafaniko yake baada ya kujifungua na kuonekana mrembo hivyo jibu ni mahabati ya mumewe.
“Sina kitu kingine chochote kinachonifanya nipendeze zaidi ya kuridhika na jinsi mume wangu anavyonijali kila siku iendayo kwa Mungu,” alisema Davina.

KIBAKA ANUSURIKA KUFA KWA KIPIGO CHA WANANCHI KAWE


Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.
Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi waliochoshwa na wizi.
...Akiendelea kusulubiwa kabla ya kupelekwa polisi.
Baada ya kulainika akawa anapelekwa polisi.
Kutokana na kipigo jamaa huyo alianguka hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa.
MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MILIONI 28 KIJIJI CHA ISNURA, MBARALI, MKOANI MBEYA


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu kulia na Meneja kampuni ya bia (TBL) Nicolaus Kanyamala wakizindua kisima cha kijiji cha Isnura 
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akimtwisha maji mwenyekiti wa kijiji cha isnura Josephine ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akiwashukuru TBL kwa kusaidia maji katika kijiji cha isnura na kuahidi kukitunza kisima hicho
Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na wakazi wa Isnura ambapo amesema kuwa TBL imekuwa na sera ya kusaidia maeneo mbali mbali hapa nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia serikali hapa nchini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Isnura  Josphine Ndimilage akisoma risala kwa niaba ya wananchi
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 28  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.